Clean-sheet za Mshery zampa jeuri Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2026
Clean-sheet za Mshery zampa jeuri Goncalves

Kikosi cha Yanga kilirejea mazoezini juzi Jumatatu kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, na kocha Pedro Goncalves wala hana presha ya kumkosa kipa namba moja Djigui Diarra, huku akiridhishwa na mrithi wake, Aboutwalib Mshery.

Diarra hataichezea Yanga kwenye mechi tatu zijazo ikiwemo mbili za ligi na moja ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kutokana na adhabu ya kusimamishwa na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kwa kumfanyia vurugu mwamuzi wa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kusimamishwa kwa Diarra hakuiumizi Yanga kwani inatamba na makipa wazuri ambao wanaweza kuziba nafasi ya Diarra wakiwemo Aboutwalib Mshery na Hussein Masalanga ambao wamekuwa wakicheza endapo kipa huyo wa Mali akikosekana.

Msimu huu kuna mechi tatu ambazo Diarra alikosekana na bado Yanga ikaendeleza ubabe kwa kushinda zote bila ya kuruhusu bao lolote ambazo alidaka Mshery.

Goncalves amesema kumkosa Diarra ni pigo lakini sio tatizo kwani haitakuwa mara ya kwanza kukosekana na Mshery amefanya vyema katika nyakati zote

“Tumeanza maandalizi ya kuendelea na mechi za ligi, tulikuwa na wachezaji wote kasoro wale ambao wako timu za taifa na wale ambao ni majeruhi, lakini kila kitu kipo sawa, tunataka kuwa tayari ili turudi njia ya ushindi,” alisema.

“Tunafahamu kwamba hatutaweza kumtumia Diarra kwenye mechi zijazo kutokana na adhabu. Sidhani kama kuna haja ya kuzungumzia uwezo wa Diarra, nadhani kila timu kuna wakati zinatamani kuwa na kipa kama huyu.”

Msimu huu Mshery amesimama golini mechi tatu dhidi ya Fountain Gate, Mashujaa na Coastal Union ambazo hakuruhusu bao na Yanga ikishinda zote.

Yanga imeruhusu mabao matatu pekee kwenye mechi zake 16 dhidi ya KMC (4-1), Dodoma Jiji (3-1) na Mtibwa Sugar (1-1) ambazo zote Diarra alikuwa langoni.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’