Mathew awaita mashabiki KMC Complex mechi dhidi ya Tanzania Prisons

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2026
Mathew awaita mashabiki KMC Complex mechi dhidi ya Tanzania Prisons

Kocha Msaidizi wa Yanga Mathew Silva amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons yamekwenda vizuri na matarajio yao ni kushinda mchezo huo utakaopigwa kesho Jumamosi, April 04 katika uwanja wa KMC Complex.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Mathew alisema timu imepata muda wa kujiandaa na mchezo huo huku wachezaji wao wakirejesha utimamu wa miili yao baada ya kipindi kigumu cha mechi mfululizo.

Mathew amesema wamejiandaa kwenda kukabiliana na mechi ngumu dhidi ya Tanzania Prisons ambayo imeonyesha kuimarika katika kila mechi.

"Tumetumia vyema kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA kujiimarisha na sasa tunaona tuko tayari kwa mechi inayokuja mbele yetu dhidi ya Tanzania Prisons"

"Tunajuma tunakwenda kukutana na mpinzani mgumu. Ukiangalia katika mechi nne zilizopita, licha ya Tanzania Prisons kutoshinda mchezo wowote, wameonyesha kuimarika," alisema Mathew

Aidha kocha huyo amesisitiza kuwa Yanga haina changamoto yoyote ya kiufundi na ndio maana timu imeendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi licha ya kupita katika kipindi kigumu cha wachezaji wao kupata majeraha yaliyotokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mazingira ya viwanja.

"Naamini hatuna tatizo lolote la kiufundi changamoto za majeraha tulizokutana nazo ni kutokana na mazingira ya baadhi ya viwanja ambavyo tunacheza. Tuna safu bora ya ulinzi na pia tuna safu bora ya ushambuliaji nafikiri tuko juu ya msimamo wa ligi si kwa bahati mbaya"

Mathew amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kuiunga mkono timu yao katika mazingira yote huku akiwataka wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo utakaopigwa saa 12 jioni.

"Natarajia kuona wananchi wakija kwa wingi uwanjani. Sio tu kuja kwa wingi, wanapaswa kushangilia ili kuipa timu hamasa. Shabiki ni nguzo muhimu kwa timu yoyote inayotafuta matokeo, nisiwe mchoyo wa fadhila kwani mashabiki wa Yanga wamekuwa nasi bega kwa bega kila tulipowahitaji. Tunafahamu mashabiki wetu wa nyumbani wanayo hamu kubwa ya kutuona,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’