Goncalves akiri Pamba Jiji wagumu, aweka mkakati wa ushindi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2026
Goncalves akiri Pamba Jiji wagumu, aweka mkakati wa ushindi

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa kesho Jumatano April 08 katika uwanja wa CCM Kirumba, utakuwa mgumu.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Pedro amesema Pamba Jiji wamejipambanua kuwa timu ngumu isiyofungika kwenye uwanja wao wa nyumbani kwani hawajapoteza mchezo nyumbani.

Licha ya ugumu huo, Goncalves amesema ana imani kubwa na kikosi chake na watakwenda kukamilisha vyema mpango wa mchezo huo na kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

"Kesho tunakutana na timu yenye ushindani mkubwa, imara wanapocheza nyumbani. Hawajapoteza mechi katika uwanja wao na timu nyingi kubwa zimekuja hapa bila kupata ushindi. Hii inaonyesha wazi ugumu wa mchezo wa kesho"

"Tunatarajia mazingira magumu ya mchezo. Uwanja hautaruhusu soka la kuvutia lakini hilo halibadilishi malengo yetu. Tunapaswa kuwa imara, makini na kupambana ili kupata alama tatu."

"Ni timu inayocheza kwa nguvu, kwa kasi na kwa msukumo mkubwa wa mashabiki wao wa nyumbani. Wanajua vizuri namna ya kutumia mazingira yao jambo ambalo linawaletea faida kubwa. Hivyo nasi tumelazimika kujiandaa kisaikolojia na kimkakati ili kukabiliana na hali hiyo"

"Huu ni msimu wa ushindani mkubwa. Kila timu inapambana kwa malengo yake, hivyo hatuna budi kuendelea kuwa makini kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha tunatumia kila nafasi tunayopata."

"Ni kweli tupo juu ya msimamo wa ligi kwa sasa na hilo linatupa morali na kujiamini. Lakini kila timu inatamani kufika hapo na muhimu zaidi ni kubaki hapo hadi mwisho wa msimu. Bado tuna michezo mingi mbele yetu hivyo safari bado ni ndefu na yenye ushindani mkubwa lakini sisi ni Young Africans na tunaamini kwenye kufikia malengo yetu na si vinginevyo"

"Nina imani kubwa na wachezaji wangu. Wameonyesha dhamira, kujituma na uwezo mkubwa wa kujifunza na kujiboresha kila siku. Kesho tunahitaji kuonyesha moyo wa upambanaji, ushindani, nidhamu na umoja ili kufanikisha malengo yetu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’