Masalanga vua kinyago, tumekustukia! we ni Diarra

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2026
Masalanga vua kinyago, tumekustukia! we ni Diarra

Jana wakati Yanga inaelekea kushuka dimba la CCM Kirumba kuikabili Pamba Jiji, yakaonekana mabadiliko eneo la mlinda lango Hussein Masalanga akianza tofauti na wengi walivyotarajia pengine mchezo huo angeanza Aboutwalib Mshery ambaye hata hivyo alipata changamoto iliyomfanya akosekane kabisa huku Semsey kutoka kikosi cha U20 akiwa golikipa wa akiba.

Lakini kazi iliyofanywa na Masalanga langoni iliwafanya Wananchi wasahau kama hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya ligi tangu alipotua kwa Wananchi kwa mkopo akitokea Singida BS kwenye usajili wa dirisha dogo.

Baada ya Diarra kukumbana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu, wapo walioamini kuwa Yanga ingeyumba eneo la walinda lango, lakini hali imekuwa tofauti.

Katika mechi zote alizokaa langoni Mshery hajaruhusu bao na Masalanga nae katika mechi yake ya kwanza pia hajaruhusu bao.

Unaweza kusema kwa sasa Yanga ina utajiri mkubwa eneo la magolikia, uwepo wa Diarra umekuwa chachu kwa walinda lango wenzake kuendeleza ubora.

Hivyo kwenye lango la Yanga kwa sasa hakuna tofauti akianza Diarra, Mshery au Masalanga! Ni mwendo wa kukusanya clean-sheet tu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’