Michuano ya CECAFA Kagame Cup inatarajiwa kuanza jijini Dar es salaam Juni 29, 2018 ikipigwa kwenye viwanja vya Taifa na Chamazi.
Kituo cha runinga cha Azam kimepewa haki ya kurusha mbashara michuano hiyo itakayochezwa sambamba na ile ya kombe la dunia inayoanza Juni 14, 2018 nchini Urusi.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amesema watahakikisha ratiba ya michuano hiyo haiathiri michuano ya kombe la dunia ili kuwapa nafasi mashabiki watakaopenda kufuatilia michuano yote.
Mshindi wa michuano ya mwaka huu atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 30,000, mshindi wa pili Dola za Marekani 20,000 na mshindi wa tatu Dola za Marekani 10,000.
Vilabu vya Yanga na Simba vimepangwa kundi C na vitachuana kwenye uwanja wa Taifa Julai 05, 2018.

ADVERTISE HERE