Yanga, GSM wapiga hatua kubwa mchakato wa ujenzi wa uwanja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2026
Yanga, GSM wapiga hatua kubwa mchakato wa ujenzi wa uwanja

Klabu ya Yanga imepiga hatua kubwa katika mchakato wa ujenzi wa uwanja wake wa kisasa, baada ya kukamilisha michoro pamoja na makadirio ya gharama za mradi huo.

Akizungumza na TBC Online, Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, alisema maandalizi ya ujenzi yanaendelea vizuri na kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa.

β€œKwenye ujenzi wa uwanja tumefika kwenye eneo zuri sana. Tunafanya mchakato wetu kwa umakini mkubwa na kwa usahihi. Tuliwatangaza GSM kuwa washindi wa tenda ya ujenzi wa uwanja. Tayari tumepata mchoro wa awali wa uwanja. Klabu imeshatoa maoni kuhusu mchoro huo. Jana tumekamilisha michoro yote na gharama za ujenzi,” alisema Hersi.

Kampuni ya GSM imepewa jukumu la kusimamia ujenzi huo, huku hatua ya kukamilika kwa michoro ikiashiria kuwa utekelezaji wa mradi unaweza kuanza mara baada ya taratibu zilizobaki kukamilika.

Uwanja huo unaotarajiwa kujengwa karibu na Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es salaam, unatarajiwa kuwa uwanja wa kisasa na wenye kukidhi viwango vya kimataifa, hatua itakayoiwezesha Yanga kuwa na uwanja wake binafsi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’