Baada ya kujihakikishia tiketi ya kutinga robo fainali kombe la CRDB, mabingwa wa soka Tanzania Yanga sasa wanahamisha nguvu zao kwenye ligi kuu ya NBC.
Alhamisi, April 16 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga watakuwa wenyeji wa KMC katika mchezo wa raundi ya 19.
Huu utakuwa mchezo wa mwisho wa ligi kwa Yanga mwezi huu kwani baada ya mchezo huu, Wananchi wataelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Muungano.
Wananchi wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kudondosha alama mbili timu hizo zilipokutana mkoani Mbeya na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Matokeo hayo yalipelekea aliyekuwa kocha mkuu Romain Folz kufutwa kazi.
Wakati huu Mbeya City watakutana na Yanga iliyoimarika zaidi, ikiwa imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 44 kutoka mechi 18Β