Ile mijadala ya wachambulizi kuhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello imemalizika rasmi baada ya Mganda huyo kuwafunga midomo kwa staili ya aina yake.
Wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC, Okello aliendelez makali yake ya kupika mabao akitoa pasi mbili za mabao.
Katika mechi mbili za ligi zilizopita, Okello ametoa pasi tano za mabao na sasa anaongoza orodha ya vinara wa asisti akiwa nazo 6.
Kwenye ligi Okello amehusika kwenye mabao nane mpaka sasa akiwa pia amepachika mabao mawili.
Yanga imeendelea kutawala kila takwimu kwani mbali na Okello, kiungo kiraka Duke Abuya nae ana asisti 5 wakati Maxi Nzengeli na Israel Mwenda kila mmoja akiwa na asisti nne.

ADVERTISE HERE