Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua jana alibeba tuzo ya nyota wa mchezo akiwaongoza Wananchi kupata ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao ulipigwa uwanja wa KMC Complex.
Katika mchezo huo ambao Yanga ilitawala kuanzia dakika ya kwanza, Pacome aliweka kambani mabao mawili huku akionyesha kiwango kikubwa.
Ni msimu wa tatu mfululizo Pacome ameendeleza ubora wake akifunga zaidi ya mabao 7 kwenye kila msimu.
Mabao yake mawili aliyofunga jana, yalimfanya afikie idadi ya mabao 7 msimu huu huku akiwa na nafasi ya kuongeza mabao zaidi katika mechi zilizobaki.
Sasa yuko nyuma kwa tofauti ya bao moja tu dhidi ya vinara wa mabao Prince Dube na Fabrice Ngoy ambao kila mmoja amefunga mabao 8.
Dube nae alipachika mabao mawili jana na hivyo kufikisha idadi hiyo ya mabao sasa akiongoza mbio za kuwania ufungaji bora.
Pacome amefunga idadi sawa ya mabao na Mudathir Yahya ambaye pia amepachika mabao 7.

