Kiungo wa Yanga Mudathir Yahya amefungiwa mechi tatu na kutoazwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi ya Bodi ya ligi baada ya kikao kilichofanyika April 18.
Mudathir anatarajiwa kukosa mechi tatu zinazofuata dhidi ya Simba, Coastal Union na KMC.
Licha ya kumkosa Mudathir hasa kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Simba, Wananchi wana uhakika na huduma ya mlinda lango Djigui Diarra ambaye adhabu yake imekwisha na kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye alikosa mechi iliyopita ya dabi ya Kariakoo iliyopigwa visiwani Zanzibar.
ADVERTISE HERE