Baada ya kukosekana kwenye kikosi cha Yanga kwa takribani mechi 5 akiuguza majeraha ya nyama za paja, mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' sasa yuko fit na pengine mashabiki wa Yanga watarajie kumuona leo katika mchezo wa robo fainali kombe la Muungano dhidi ya Muembe Makumbi.
Depu alianza vyema majukumu yake na Yanga kabla ya kukumbana na majeraha hayo yaliyomuweka nje kw takribani wiki tatu.
Katika mechi zake 10 za kwanza alizoitumikia Yanga, Depu alifunga mabao 11, mabao 6 ameyafunga kwenye ligi kuu ya NBC.
Bila shaka mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves atampa nafasi kubwa kwenye michuano hii ya kombe la Muungano ili aimarishe 'fitness' yake kabla ya mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa May 03.
Wakati Depu akisubiriwa kurejea uwanjani, mshambuliaji mwenzake Prince Dube ambaye pia alikuwa majeruhi kwa wiki kadhaa, yeye yuko fit na ameendeleza pale alipoishia mara ya mwisho baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya Mbeya City.