Pedro awatumia salamu wapinzani wake kombe la Muungano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2026
Pedro awatumia salamu wapinzani wake kombe la Muungano

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ameweka wazi dhamira yake ya kutetea taji la Muungano leo wakicheza mchezo wa robo fainali dhidi ya Muembe Makumbi.

Pedro ambaye hii ni mara yake ya pili kuiongoza Yanga kwenye mashindano yanayofanyika visiwani Zanzibar baada ya mapema mwaka huu kuwaongoza Wananchi kutwaa taji la Mapinduzi, amesema kikosi chake kimejipanga kucheza mechi zote tatu za michuano hiyo kwa maana ya kufika hadi fainali.

Concalves aliwasili Zanzibar jana akiwa na kikosi chake kamili ambapo wachezaji ambao hawakusafiri ni wale walio majeruhi.

“Tumefika hapa, kama ilivyo kawaida hii ni timu ambayo wakati wote inahitaji mafanikio, tumekuja kama bingwa mtetezi, tunataka kuendeleza yale ambayo tuliyafanya msimu uliopita"

“Nilikuwa hapa wakati wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi, najua namna ilivyo ngumu kushinda dhidi ya timu za hapa, hatuwezi kuchukulia rahisi timu ya Mwembe Makumbi.

“Tumekuja na timu kamili, wachezaji ambao tumewaacha nyuma ni wale ambao tunaona sio rahisi sana kucheza msimu huu lakini wengine wote wako hapa tutakuwa na mechi tatu mpaka kufika fainali,” alisema Pedro.

Aidha Pedro amesema Yanga haiwezi kuogopa mpinzani yeyote ambapo kikosi chake kitacheza kwa kiwango kikubwa kulingana na ubora wa mpinzani aliye mbele yao wakitumia ubora wao.

“Hakuna nafasi ya kuhofia timu yoyote unapokuwa unafanya kazi na timu kama hii ya Yanga, tuna wachezaji waliokomaa, wanajua namna ya kucheza mechi za presha, tutawaheshimu wapinzani ambao tutakutana nao, kila timu tutakuwa na mpango wa kucheza nayo,” aliongeza Pedro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’