Hawataamini macho yao Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2026
Hawataamini macho yao Jumatano

Yawezekana kuna watu bado wana picha ya ile Yanga ya March 1 iliyokuwa 'dhoofu' kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Kila Mwanayanga hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao katika mchezo huo ambao unaweza kusema ndio umewapa jeuri watani zao Simba kuamini sasa wanaubavu wa kuchuana na mabingwa hao wa kihistoria.

Baada ya Simba kutinga fainali ya ligi ya Muungano jana, utaona tambo zimekuwa nyingi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo wakiamini wanakwenda kupata ushindi mwepesi dhidi ya Yanga lakini ukweli ni kuwa hawajuia wanachokwenda kukutana nacho.

Baada ya sare dhidi ya Simba na kufuatiwa na sare nyingine dhidi ya Azam Fc, TRA United na Mtibwa Sugar, uongozi wa Yanga ulichukua hatua muhimu kuirejesha timu kwenye ubora wake.

Hatua hizo ndizo zilizoifanya Yanga leo ionekana kuwa bora mara dufu na hata kupelekea baadhi ya wachambuzi kuanzisha propaganda kuwa wananunua mechi.

Baada ya kile kikao kilichokuja na maamuzi ya kuongeza nguvu benchi la ufundi wakimrejesha Kocha Msaidizi Abduhamid Moalin, huo ulikuwa mwanzo wa kusukwa Yanga mpya ambayo sasa iko kwenye kilele cha ubora.

Tangu wakati huo Yanga imeshinda mechi sita katika mashindano yote huku ikifunga mabao 19 na kuruhusu bao moja tu. Katika vipigo walivyotoa ni TMA Stars na Azam Fc waliofungwa mabao machache, wengine wote wamefungwa kuanzia mabao matatu tena bila ya wao kuzitikisa nyavu za Wananchi.

Tanzania Prisons (3-0), Pamba Jiji (3-0), Mbeya City (6-0) na Muembe Makumbi (4-0). Ni Yanga iliyoimarika zaidi katika eneo la ushambuliaji lakini pia ikiendeleza ubora katika safu ya ulinzi.

Ni wazi April 29 inaweza kuwa siku nyingine ya kuandikwa historia kwenye mechi za dabi ya Kariakoo mpaka sasa Yanga ikiwa imecheza mechi 7 mfululizo bila ya kupoteza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’