FT : Simba 2-2 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 May 2026
FT : Simba 2-2 Yanga, NBC PL

Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Zilikuwa dakika 90 ngumu zilizohitaji ujasiri na moyo wa kupambana, Yanga ikitokea nyuma kwa mabao 2-0 kupata sare.

Dakika ya pili tu Yanga iliruhusu bao la kwanza mfungaji akiwa Libasse Gueye baada ya makosa ya mlinzi wa kulia Israel Mwenda aliyenyang'anywa mpira wakati Yanga ikitengeneza shambulzi kutokea nyuma.

Bao hilo ni kama liliwachanganya Yanga na kujikuta wakiruhusu bao la pili dakika chache baadae mfungaji akiwa ni Clatous Chama.

Baada ya kuingia kwa bao hilo Yanga waliamka na kwenye dakika ya 18 Prince Dube akarejesha bao moja baada ya pasi ya Duke Abuya ndani ya eneo la hatari.

Vijana wa kocha Pedro Goncalves waliendelea kushambulia wakisaka bao la kusawazisha lakini dakika 45 za kwanza zilimalizika wakiwa nyuma.

Kipindi cha pili Yanga ilirejea na kasi kubwa na kufanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 50 kupitia kwa nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto aliyemalizia mpira uliotemwa na mlinda lango Djibrill Kassali.

Pengine Yanga ingeweza kuondoka na ushindi kwani kulikuwa na nafasi zilizopotezwa hasa ya Dube dakika ya 76.

Sare hii kwa Yanga ni kama ushindi kwa kuzingatia ugumu wa mchezo huo pamoja na hali ya uwanja w Isamuhyo.

Hivi ndio timu bingwa inapaswa kucheza, ukikosa ushindi katika mechi kubwa chukua hata alama moja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’