Baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba hapo jana, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani ratiba inaendelea.
Jumatano, May 06 Yanga itashuka uwanja wa KMC Complex kuchuana na wenyeji wao KMC katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.
Unaweza kusema hii ni dabi ya dimba la KMC Complex kwani timu zote zinatumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani.
Wananchi wanahitaji alama tatu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.
Baada ya mchezo huo, May 09 Yanga itarudi tena KMC Complex kuikabili Coastal Union na kisha kuelekea mkoani Singida kuikabili Dodoma Jiji mchezo utakaopigwa May 13 uwanja wa Airtel.
May 22 Wananchi watakuwa tena KMC Complex kuikabili Singida BS na May 25 kuikaribisha Namungo Fc katika uwanja huo
ADVERTISE HERE