Matchday; KMC vs Yanga, NBC PL, May 06

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2026
Matchday; KMC vs Yanga, NBC PL, May 06

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 21 ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa uwanja wa kMC Complex kuwakabili wenyeji wao KMC katika mchezo unaozikutanisha timu zenye malengo tofauti.

Wakati Yanga ikiwania alama tatu muhimu ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi, KMC wanaburuza mkia na pengine inaweza kuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu.

Wakusanya ushuru hao wa Kinondoni wamekusanya alama 9 kutoka mechi 20, kimahesabu wanahitaji kushinda kila mchezo ili kuwa salama.

Bahati mbaya kwao ni kuwa wanakutana na Yanga ambayo macho imeelekeza kwenye ubingwa, ikihitaji kuchukua alama tatu kwenye kila mchezo ili kuhakikisha wanakamilisha malengo yao.

Baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba katika mchezo uliopita, nyota wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja ambapo jana walikamilisha maandalizi yao kuelekea mchezo huo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi waipe sapoti timu yao katika mchezo ambao alama tatu ni muhimu sana kwao.

Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’