Thank You ya Goncalves lilikuwa suala la muda tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2026
Thank You ya Goncalves lilikuwa suala la muda tu

Hatimaye jana Yanga ikatangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu Pedro Goncalves muda mfupi baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC.

Goncalves alisimamia mchezo huo uliopigwa uwanja wa KMC Complex akishuhudia kikosi chake kikiibuka na ushindi wa bao 1-0. Hata hivyo punde si punde akakutana na taarifa kwa UMMA, kibarua chake kimeota nyasi.

Wadadisi wa mambo wanasema uamuzi huu ulichukuliwa muda mrefu pengine ulikuwa ukisubiri wakati mwafaka ili ukamilishwe.

Baada ya zile sare tatu mfululizo mwezi March, mabosi wa Yanga walikutana wakihitaji maelezo kutoka benchi la ufundi juu ya mfululizo huo wa matokeo mabovu.

Baada ya kikao kile, maazimio yalifikiwa kumleta kocha Msaidizi Abdulhamid Moalin kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi baada ya kubaini Yanga ilikuwa imepoteza radha yake ya kiucheza chini ya Goncalves.

Uongozi wa Yanga uliihifadhi 'Thank You' ya Goncalves kwa wakati ule wakimpa nafasi nyingine wakiamini akishirikiana na Moalin mambo yanaweza kubadili.

Na kweli ujio wa Moalin ukaleta mabadiliko chanya kwenye kikosi licha ya kuwa Goncalves aliendelea kushikilia misimamo yake ya kimbinu.

Yakaanza kusikika malalamiko kutoka kwa Wanayanga juu ya uamuzi wa kocha huyo kutowatumia baadhi ya wachezaji akiwemo Yao Kouassi ambaye wengi walishangazwa kuwekwa nje kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Muungano.

Moja ya maelekezo ambayo uongozi wa Yanga ulitoa kwa benchi la ufundi ni pamoja kuwatumia wachezaji wote kwa kuzingatia mahitaji ili kulinda viwango vyao kwani kulikuwa na wachezaji walikosa nafasi hata kwenye mechi ndogo na kupelekea baadhi ya wachezaji kutumika mfululizo na kuwapelekea changamoto za majeruhi.

Goncalves aliiongoza Yanga katika mechi 19 za ligi akishind 14 na kutoka sare mechi 5. Ni wazi kilichomuondoa Yanga kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na maamuzi yake binafsi kwenye usimamizi wa timu na kuamini zaidi katika mbinu zake kuliko kile ambacho Wanayanga walihitaji kuona.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’