Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello jana aliendelea kudhihirisha thamani yake ndani ya kikosi cha Wananchi.
Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Uganda alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Pamoja na kufunga, Okello pia alitoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Maxi Nzengeli na hivyo kuondoka na tuzo ya nyota wa mchezo baada ya dakika 90 kukamilika.
Okello sasa amefikisha mabao matano huku pia akifikisha pasi saba za mabao amehusika kwenye mabao 12 yaliyofungwa na Yanga.
Ikumbukwe Okello amejiunga na Yanga mwezi Januari kwenye usajili wa dirisha dogo. Pengine ndio mchezaji aliyechangia mabao mengi kwenye ligi tangu Januari.
ADVERTISE HERE