Ilikuwa siku mbaya ofisini kwa kapteni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2026
Ilikuwa siku mbaya ofisini kwa kapteni

Siku kama ya leo inapaswa kuondoka haraka kwenye vichwa vya wachezaji ili kuhakikisha wanarejea wakiwa imara kwenye mchezo unaofuata.

Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ni miongoni mwa wachezaji wanaopaswa kusahau mchezo huu haraka.

Unaweza kusema mabao mawili ya kwanza waliyofunga Dodoma yalichangiwa na kukosekana kwa umakini kati ya nahodha na walinda lango wake.

Bao la kwanza Mwamyeto alijifunga katika jitihada za kuokoa mpira ambao alikuwa na nafasi ya kufanya maamuzi bora zaidi.

Bao la pili hakuwa na mawasiliano mazuri kati yake na golikipa Masalanga, alimpoteza golikipa baada ya kukwepa mpira ambao alikuwa na uwezo wa kuondoa kwa kichwa.

Dodoma Jiji hawakuwa na mashambulizi mengi langoni kwa Yanga lakini unaweza kusema walizawadiwa mabao mawili ambayo waliwarahisishia kazi.

Eneo la safu ya ushambuliaji pia hawawezi kukwepa lawama kwani nafasi nyingi zilipotea. Yanga ilikuwa na uwezo wa kumaliza mechi mapema kama nafasi zingetumika kwa usahihi.

Prince Dube hii ilikuwa mechi kuchukua usukani kwenye mbio za ufungaji bora lakini hakuwa katili mbele ya lango.

Kwenye mpira wa miguu kama hutumii nafasi unampa ujasiri mpinzani wako na kumuweka mchezoni. Ndicho kilichotokea leo Dodoma Jiji wakiibuka na ushindi wa mabao 3-2 baada ya 'kukoswa na mishale mingi'.

Nguvu sasa zielekezwe kwenye mchezo wa robo fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa Jumamosi, May 16 uwanja wa Isamuhyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’