Siku za karibuni zimeibuka propaganda zinazomuhusu beki wa Yanga Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' ambaye hajaonekana uwanjani kwenye mechi kadhaa zilizopita kutokana na changamoto ya majeraha.
Meneja wa mchezaji huyo Carlos Mastermind amejitokeza kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo akisisitiza kuwa hakuna changamoto yoyote baina ya uongozi wa Yanga na Zimbwe Jr.
Carlos amethibitisha kuwa Zimbwe Jr hana madai yoyote kwa uongozi wa Yanga kwani fedha zake zote za usajili alishalipwa.
"Napokea simu nyingi na sms kuhusu hii kitu, Mohammed alipata majeraha kwenye mechi ya Ligi dhidi ya Mbeya City pale KMC Complex na club ilitoa hii statement, anaendelea na matibabu vizuri hajawa 100% Fit."
"Mohammed haidai club, Yanga paid 100% of his Signing-on Fees and all the agreed renumeration. Heβs very Happy with the new Environment," aliandika Carlos kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akimaanisha Yanga ililipa kwa asilimia 100 makubaliano yote ya fedha za usajili.