Yanga vs Singida BS ni kama fainali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2026
Yanga vs Singida BS ni kama fainali

Ijumaa May 22 uwanja wa KMC Complex Yanga itaikaribisha Singda BS katika mchezo wa raundi ya 24 ligi kuu ya NBC.

Ni moja mechi ngumu zilizobaki kwa Yanga katika kutimiza mkakati wake wa kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji, ni wazi hakuna tena nafasi ya kufanya makosa kwa Wananchi katika mechi zilizobaki.

Wananchi wanahitaji alama tatu kwenye kila mchezo wakianza na Singida BS ambayo haijawahi kuwa mpinzani mwepesi kila inapokutana na Yanga.

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa mkoani Singida lakini haukuwa mchezo mwepesi.

Ufanisi na kutumia nafasi kwa usahihi ndio kilichopelekea Yanga kushinda mchezo huo. Wananchi wanapaswa kurudia kila walichofanya Sngida ili kuibuka na ushindi.

Singida BS tayari wako jijini Dar es salaam wakijiandaa na mchezo huo huku msemaji wao Hussein Masanza akitamba kuwa wamekuja Dar kuchukua alama tatu.

Yanga imeingia kambini leo kukamilisha maandalizi ya mtanange huo ambao Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’