Licha ya kujiunga na Yanga Januari kwenye usajili wa dirisha dogo, kiungo mshambuliaji Allan Okello amepanda hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya vinara wa ufungaji mabao msimu huu akifikisha mabao 9 sawa na Prince Dube.
Okello jana aliweka kambani mabao mawili na kufikisha 9 huku pia akiwa ametoa pasi 7 za mabao akihusika katika jumla ya mabao 16.
Nyota huyo wa Kimataifa kutoka Uganda amekuwa kwenye 'form' nzuri ya kuzifumania nyavu, mabao matatu nyuma ya Feisal Salum mengi.

ADVERTISE HERE