Matchday; Yanga vs Namungo Fc, NBC PL, May 25

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2026
Matchday; Yanga vs Namungo Fc, NBC PL, May 25

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo raundi ya 25 ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watashuka dimba la KMC Complex kuikabili Namungo Fc.

Ni mchezo mwingine muhimu kwa Wananchi kusaka alama tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi.

Baada ya watani zao Simba kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji jana, Yanga haipaswi kupoteza mchezo dhidi ya Namungo Fc ili kurejea kwenye nafasi yao.

Hautakuwa mchezo mwepesi kwa Yanga, historia inaonyesha mechi zinazokutanisha timu hizo huwa ni ngumu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mechi hiyo ni kama 'dabi ndogo' akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao.

Yanga leo itaingia kwenye mchezo huo bila ya kiungo wake mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye alipata majeraha ya goti katika mchezo uliopita dhidi ya Singida BS.

Hata hivyo mkufunzi wa Yanga Abdihamid Moalin amesema majeraha hayo sio makubwa sana na hivyo nyota huyo raia wa Ivory Coast atarejea dimbani mapema.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 jioni..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’