Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kama sio takwimu, mchezaji anayestahili kushinda tuzo ya MVP msimu huu ni Duke Abuya.
Abuya amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu ambapo jana aliwaongoza Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Abuya alifunga bao la kwanza la Yanga baada ya shambulizi la kushitukiza alilolianzisha yeye mwenyewe kutokea nyuma na kwenda kumaliza.
Kamwe amesema nyota huyo raia wa Kenya amekuwa na msimu bora kwa kile anachokifanya uwanjani.
"Kama tuzo ya MVP ingetolewa bila kuzingatia takwimu, basi ningesema Duke Abuya anastahili tuzo ya MVP"
"Lakini kwa sababu kinachoangaliwa ni namba, kama ligi inaisha leo, tuzo hiyo atastahili Feisal Salum."
"Allan Okello ameingia dirisha dogo kwa sasa jukumu lake ni kuisaidia Yanga kutetea taji kwa msimu mwingine."
"Labda kama atafanya vyema zaidi kwenye mechi zilizobaki na kuwa na namba nzuri kuliko Feisal, anaweza kuwania tuzo hiyo," alisema Kamwe.
Akicheza maeneo tofauti uwanjani kulingana na mahitaji ya mechi, Abuya ameendelea kufanya vyema, unaweza kusema ndio injini ya Yanga pale kati.. Amefunga mabao matatu na kutoa pasi 6 za mabao