Nyota wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima ameendelea kuhudhuria mafunzo ya ukocha akiwa hatua chache kuwa kocha kamili.
Hivi karibuni Niyonzima ameshiriki mafunzo shule ya soka ya Atletico Madrid akipata nafasi ya kujifunza kutoka kwa mshambuliaji nguli wa Hispania Fernando Torres ambaye kwa sasa anawanoa vijana wa Atletico Madrid B.
Niyonzima amepata sapoti kubwa kutoka chama cha soka Rwanda katika kuhakikisha anafikia ndoto yake ya kuwa mkufunzi.
Niyonzima aliitumikia Rwanda kwa mafanikio makubwa wakati huu nae anapata fadhila kutoka kwa Tafa lake.
Moja ya ahadi zake wakati anaondoka Yanga, Niyonzima alisema siku moja atarejea tena Yanga akiwa kocha.
Unaweza kusema mpaka sasa anaishi katika ndoto yake na pengine yuko karibu sasa kufikia matarajio yake.


