Kwa Girumugisha tatizo ni dau la usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2026
Kwa Girumugisha tatizo ni dau la usajili

Klabu ya Yanga SC inaendelea kuhusishwa na mpango wa kumsajili winga hatari wa klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan, Jean Claude Girumugisha.

Mchezaji huyo raia wa Burundi mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akivutia macho ya mabingwa hao wa Tanzania kutokana na kiwango chake kikubwa cha ubunifu, kasi na uwezo wa kucheza nafasi zote za winga kwa ufanisi.

Uongozi wa Yanga SC kupitia Rais wake Eng. Hersi Said unatajwa kuwa umeshaanza kufuatilia upatikanaji wa mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo, changamoto kubwa katika dili hilo inaelezwa kuwa ni gharama ya usajili. Inasemekana kuwa dau la kumtoa Girumugisha linaweza kufikia zaidi ya dola za Marekani milioni moja (USD 1M), kiwango ambacho huenda kikahitaji Yanga “kuvunja benki” ili kukamilisha usajili huo.

Girumugisha, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji chipukizi wanaofuatiliwa kwa karibu barani Afrika, bado ana mkataba wa muda mrefu na Al Hilal Omdurman na amekuwa akionesha kiwango bora katika michuano ya CAF, jambo linaloongeza thamani yake sokoni.

Kwa upande mwingine, Yanga SC inaendelea na mpango wake wa kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao, ambapo usajili wa mchezaji wa kiwango cha Girumugisha ni aina za sajili zinazohitajika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’