Inaelezwa uongozi wa klabu ya Yanga umefikia makubaliano ya pande mbili kusitisha mikataba ya nyota wake waliokuwa kwa mkopo Ecua Celestin na Mohamed Doumbia.
Ecua alitolewa kwa mkopo klabu ya JS Kabylie kwa makubaliano ya kumnunua moja kwa moja kama wataridhishwa na uwezo wake.
Hata hivyo Kabylie wameamua kutoendelea nae huku Yanga pia ikiwa haina mpango wa kuendelea nae.
Yanga pia imeachana na Doumbia ambaye pia alitolewa ka mkopo klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Kuelekea kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili, kuna maboresho makubwa Yanga inatarajiwa kufanya hasa usajili wa nyota wa kigeni.
Kuna taarifa pia Yanga itaachana na winga Buba Jammeh ambaye alitua kwa Wananchi katika dirisha dogo la usajili.
ADVERTISE HERE