Beki wa kulia wa Yanga Israel Mwenda miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo inaelezwa Yanga haijafungua mazungumzo yoyote ya kuhuisha mkataba wake huku kukiwa na taarifa kuwa tayari amemalizana na waajiri wake wa zamani Singida BS.
Mwenda ameitumikia Yanga kwa misimu miwili hata hivyo majeraha ya mara kwa mara yamemfanya akose baadhi ya mechi kuelekea mwishoni mwa msimu.
Aidha kuimarika kwa Yao Kouassi 'Jeshi' ni sababu nyingine iliyomfanya Mwenda apoteze nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.
Katika mechi za karibuni, benchi la ufundi la Yanga limewatumia Yao na Kibwana Shomari zaidi huku Mwenda akipata dakika chache.
ADVERTISE HERE