Moalin aweka wazi Yanga haitishwi na maneno, inataka alama tatu Kigoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2026
Moalin aweka wazi Yanga haitishwi na maneno, inataka alama tatu Kigoma

Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Moalin amesema baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA, wachezaji wamerejea wakiwa na ari, morali kubwa dhamira yao ikiwa kushinda mchezo huo.

Moalin amesema wanaiheshimu Mashujaa Fc lakini wao wako Kigoma kuzitafuta alama tatu ili kulinda malengo ya msimu huu ambayo ni kutwaa ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo.

"Kwanza kabisa, maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea mchezo wa kesho. Tulikuwa na kipindi kizuri cha dirisha la FIFA ambapo tulipata muda mzuri wa maandalizi. Ninafurahi kuona Wachezaji wangu wana hamasa kubwa na wako tayari kurejea kwenye mechi za mwisho za NBC Premier League, tukianza na mchezo wa kesho dhidi ya Mashujaa FC"

"Mashujaa ni timu nzuri na tunawaheshimu sana, kama tunavyoheshimu wapinzani wetu wote. Hata hivyo, sisi tuko tayari na tunajua kile tunachopaswa kufanya. Tunajua kwa nini tumekuja Kigoma na tuko kwenye dhamira maalum. Dhamira yetu kwa sasa ni mchezo wa kesho na tumejikita kuhakikisha tunapata alama tatu"

"Hakuna mchezo rahisi katika ligi hii. Haijalishi tunacheza na timu ya mwisho kwenye msimamo au timu ya pili, kila mchezo kwetu ni fainali. Lengo letu ni kutwaa ubingwa wa tano na kila mchezo ni hatua muhimu kuelekea kufanikisha azma hiyo."

"Iwapo tutashinda kwa mabao mengi au machache si jambo la msingi. Kilicho muhimu ni kupata ushindi na alama tatu. Wachezaji wetu ni wenye uzoefu mkubwa lakini pia ni wanyenyekevu sana. Licha ya mambo mbalimbali yanayosemwa nje ya uwanja, wao wamebaki wakifanya kazi kwa bidii kila siku. Wengine wanapigania ubingwa wao wa tano, wengine wa pili na wengine wa kwanza, lakini wote wana njaa ya kumaliza msimu huu kwa nguvu," alisema Moalin

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’