FT : Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup SF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2026
FT : Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup SF

Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la CRDB baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.

Ulikuwa mchezo ambao unaweza kusema makosa kwenye safu ya ulinzi ya Yanga ndio yaliwagharimu kwani waliruhusu kufungwa mabao mepesi.

Himid Mao alitangulia kufunga bao la uongozi kwa mpira wa kichwa baada ya walinzi wa Yanga kuzembea kuondoa mpira wa hatari langoni.

Azam Fc ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Alikuwa ni Prince Dube aliyesawazisha bao kupitia mpira wa kichwa baada ya krosi ya Allan Okello.

Makosa mengine yakaigharimu Yanga dakika ya 85 Lameck Lawi akifunga kwa mpira wa kichwa baada ya kona ya Feisal Salum.

Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto akairejesha Yanga mchezoni dakika tatu baadae akifunga kwa kichwa baada ya krosi kutoka kwa Okello.

Bao hilo lililazimishwa mchezo kwenda muda wa nyongeza dakika 30. Yanga ilirejea kwa nguvu kubwa ikisaka bao la ushindi dhidi ya Azam Fc waliokuwa pungufu baada ya beki Yoro Diaby kutolewa nje kwa kadi nyekundu alipomzuia Dube aliyekuwa anaelekea kufunga.

Mashambulizi mfululizo langoni kwa Azam Fc yaliishia mikononi mwa golikipa Zuberi Foba huku wainzi wa timu hiyo wakifanya kazi kubwa kubaki mchezoni.

Makosa mengine kutoka kwa Bacca yakaigharimu Yanga dakika tano za mwisho akirudisha mpira mfupi kwa golikipa ambao aliuwahi mshambuliaji Japhet Kitambala na kuujaza kimiani.

Baada ya miaka minne ya kutawala taji la CRDB hatimaye ufalme huo umefika tamati leo na sasa Yanga inahitaji kupambana kutetea taji la ligi kuu lililobaki.

Watachuana tena na Azam Fc Jumatano Juni 24 uwanja wa New Amaan Complex katika mchezo wa ligi kuu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’