Keshokutwa Jumatano, Wananchi Yanga watashuka dimba la New Amaan Complex kuikabili Azam Fc kwenye mchezo muhimu wa ligi kuu ya NBC.
Mchezo huu ni kama fainali, Yanga inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo.
Ni mtanange unaotizamwa kwa jicho tofauti kwani unaweza kuamua mbio za ubingwa mapema.
Kikosi cha Yanga tayari kimewasili visiwani Zanzibar kuelekea mtanange huo wanaohitaji ushindi kwa gharama yoyote.
Tayari viingilio vimewekwa hadharani huku Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe akiwataka mashabiki kununua tiketi kwa wingi ili kujaza dimba la New Amaan Complex.

ADVERTISE HERE