Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jun 2026
Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Azam Fc

Mkufunzi wa Yanga Abdihamid Moalin amesema wamejiandaa kukamilifu kukabiliana na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa New Amaan Complex.

Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo, Moalin amesema wanatambua hautakuwa mchezo rahisi lakini wamejiandaa vyema kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

"Tunashukuru tulikamilisha vyema mchezo uliopita, hatukuwa na majeruhi hivyo tunajiandaa kikamilifu kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc."

"Tunatambua utakuwa mchezo mgumu kwani tunakwenda kucheza dhidi ya timu bora yenye wachezaji na kocha bora."

"Kila mchezo kwetu ni fainali kwa sababu malengo yetu ni kutetea taji la ligi kuu, licha ya ugumu wa ratiba, ni jukumu letu kupambana na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye kila mechi."

"Tumecheza na Azam Fc siku chache zilizopita, hilo linatupa mwanga wa maandalizi kuelekea mchezo huu. Tutaendeleza mazuri tuliyofanya katika mchezo uliopita na pia kusahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita, "alisema Moalin.

Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya Azam Fc ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’