FT : Yanga 3-0 Azam Fc, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2026
FT : Yanga 3-0 Azam Fc, NBC PL

Waliyemtuma kashindwa kazi! Ndio unavyoweza kusema baada ya Yanga kuiadhibu vikali Azam Fc Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Ulikuwa mchezo ambao wachezaji wa Yanga walifahamu tangu dakika ya kwanza kuwa wanahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri kutetea ubingwa.

Baada ya kosakosa nyingi kipindi cha kwanza, alikuwa ni Ibrahim Bacca aliyefunga bao la utangulizi dakika ya 41 akimalizia kwa kichwa mpira wa Prince Dube.

Yanga iliyotawala mchezo huo, ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Azam Fc waliamka wakisaka bao la kusawazisha hata hivyo haikuwa rahisi kwao kumdhibiti Laurindo Aurellio 'Depu' ambaye kwenye dakika ya 73 aliifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Msumari wa mwisho kwenye jeneza la Azam Fc ulipigiliwa na Pacome Zouzoua kwenye dakika ya 81 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango Zuberi Foba baada ya shuti la Dube.

Ni ushindi muhimu kwa Yanga kuelekea mechi mbili za kumaliza msimu ambapo sasa Wananchi wanahitaji angalau alama nne tu ili kutetea ubingwa.

Katika nyakati ambazo wengi waliamini mambo yatakuwa magumu kwa Yanga, kwa mara nyingine wananchi wamedhihirisha bado ndio timu bora nchini na wanastahili kuwa katika nafasi waliyopo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’