FT : Yanga 3-0 TRA United, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jun 2026
FT : Yanga 3-0 TRA United, NBC PL

Yanga imetakata uwanja wa KMC Complex ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa mzunguuko wa 29.

Yanga iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na ari ya kuhitaji matokeo ya ushindi na kazi ilifanywa vyema na Allan Okello 'Star Boy' aliyefunga hat-trik ya nne msimu huu.

Okello alifunga bao la uongozi la Yanga dakika y 27 akimalizia krosi ya Prince Dube na kuipeleka Yanga mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga iliendeleza msako kwenye lango la TRA United wakifanikiwa kupata mkwaju wa penati kwenye dakika ya 51 baada ya mlinzi wa TRA United kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Okello alikamilisha hat-trik yake dakika ya 57 baada ya Yanga kufanya shambulizi kali kutoka upande wa kushoto Okello akikutana na mpira unaozagaa eneo la hatari na kuuweka kambani.

Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi na pengine Yanga ingefunga mabao zaidi kama umakini ungekuwa mkubwa eneo la umaliziaji.

Ushindi huo unaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya JKT Tanzania pengine wakihitaji alama moja tu kumaliza kazi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’