Yanga Bingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2026
Yanga Bingwa

Yanga imeweka rekodi ya aina yake baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tano mfululizo.

Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Isamuhyo umewahakikishia Wananchi ubingwa wa 32 katika historia yao.

Prince Dube ndiye aliyefungua kalamu ya mabao akifunga bao la mapema dakika ya 9 ambalo liliwapeleka Wananchi mapumziko wakiwa mbele.

Hata hivyo ilikuwa huzuni kwa mashabiki wa Yanga pale waliposhuhudia kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua akipata majeraha mabaya mwishoni mwa kipindi cha kwanza tukio ambalo lilipeleka beki wa JKT Tanzania Twalib Hassan kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo na kuongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Maxi Nzengeli na Laurindo Aurelio 'Depu'.

Ama kwa hakika ulikuwa msimu wenye misukosuko ya hapa na pale lakini kwa mara nyingine Yanga imeweza kuibuka kidedea na kuandikisha historia.

Pongezi kwa benchi la ufundi kuanzia Romain Folz, Pedro Goncalves na Abdihamid Moalin na wenzake ambao wameweza kukamilisha vyema malengo pale walipokabidhiwa majukumu

Ari na moyo wa upambanaji hata katika nyakati ambazo wengi walipoteza matumaini, zimewapa zawadi kubwa ya ubingwa mwishoni.

YANGA BINGWAAAAAAA...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’