Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto kwa mara ya tano mfululizo leo amenyanyua taji la ligi kuu ya NBC.
Ni baada ya Yanga kusepa na ubingwa baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania na kuwapiku watani zao Simba kwenye mbio za ubingwa.
Hii ni rekodi katika kizazi hiki, Yanga inakuwa klabu ya kwanza kutwaa taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.
Zipo rekodi za miaka ya 70 kwa Yanga na Simba kushinda taji hilo mara tano lakini Yanga imerudia rekodi katika kizazi hiki ambacho ushindani umeongezeka kwani klabu zinafanya uwekezaji mkubwa.
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameendelea kuishi katika ahadi zake, ameiwezesha Yanga kushinda mataji matano mfululizo na rasmi kusimika utawala kwnye soka la Tanzania.
Ubingwa huu utawauma saaaana....!