Ama kwa hakika tukio la kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua kuumizwa vibaya wakati akiipambania Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania, limewapa simanzi mashabiki na wadau wa soka nchini.
Pacome alifanyiwa rafu mbaya sana na beki wa JKT Tanzania Twalib Hassan mwishoni mwa kipindi cha kwanza tukio ambalo lilipelekea Pacome kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya huduma ya dharura.
Licha ya kuwa bado taarifa rasmi haijatolewa na uongozi wa Yanga juu ya aina ya jeraha na muda ambao anaweza kuwa nje, kwa hakika ni jeraha kubwa ambalo linaweza kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Yanga imeutoa ubingwa kama 'dedication' kwa Pacome na wachezaji wengine Dickson Job, Clement Mzize, Aboubakar Khomein ambao walipata majeraha makubwa msimu huu wakiwa wanaipambania Yanga.
Get well soon Pacome..!