Mossi kumrithi Dube Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2026
Mossi kumrithi Dube Yanga?

Baada ya mshambuliaji Prince Dube kujiunga rasmi na Hardrock FC ya Zimbabwe, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameanza mchakato wa kutafuta mbadala wake, huku jina la Ndumumwe Mossi likitajwa kuibuka kama chaguo la kwanza.

Dube aliondoka Yanga jana kuelekea klabu yake ya nyumbani Zimbabwe baada ya kumalizika kwa mkataba wake, hatua iliyowashangaza mashabiki wengi kutokana na klabu hiyo kuwa katika mchakato wa kumshawishi kuongeza mkataba mpya.

Hata hivyo, kuondoka kwake kumeacha pengo katika safu ya ushambuliaji ya Yanga, na sasa uongozi umeanza harakati za kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, mabosi wa klabu hiyo tayari wameanza mawasiliano ya awali na Singida Big Stars (Singida BS) kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji hatari Ndumumwe Mossi.

Mossi, raia wa Burundi, alijiunga na Singida BS mwezi Januari 2026 katika dirisha dogo la usajili, na ndani ya muda mfupi ameonyesha ubora mkubwa uliomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia zaidi katika msimu uliomalizika.

Nyota huyo aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufunga mabao 17, akiwa pia mchezaji pekee aliyefanikiwa kufunga hat-trick mbili katika msimu mmoja, hatua iliyosaidia Singida BS kumaliza nafasi ya nne na kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu ujao.

Silaha kubwa ya Mossi ni ufanisi wake mbele ya lango, ambapo anajulikana kama mshambuliaji asiyehitaji nafasi nyingi kufunga mabao. Uthibitisho wa ubora wake ni rekodi yake ya mabao 17 katika mechi 21 alizochezea Singida BS.

Uongozi wa Yanga unaonekana kuvutiwa na uwezo wake wa kumalizia nafasi, jambo linaloonekana kuwa kipaumbele baada ya kuondoka kwa Dube, ambaye licha ya umahiri wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja kwenye safu ya ushambuliaji, ufanisi wake mbele ya lango uliibua mijadala mara kwa mara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’