Fadlu anaweza kutua kama utani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2026
Fadlu anaweza kutua kama utani

Aliyekuwa kocha wa Raja CA, Fadlu Davids, anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu kuelekea msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Afrika Kusini iDiski Times, Yanga wamewasilisha ofa rasmi kwa kocha huyo raia wa Afrika Kusini, taarifa zaidi zikibainisha Fadlu ameridhia kutua Yanga mazungumzo yakiwa kwenye hatua ya majadiliano ya kimkataba.

Iwapo dili hilo litakamilika, litakuwa moja ya hatua zitakazozua mjadala mkubwa katika soka la Tanzania kutokana na historia ya Davids ndani ya klabu pinzani ya Simba SC.

Davids aliinoa Simba katika msimu wa 2024/25 na kuifanya irejee kwenye ushindani mkubwa wa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Chini yake, Simba ilimaliza ligi wakiwa nyuma kwa pointi nne pekee dhidi ya Yanga, huku mbio za ubingwa zikiamuliwa katika mchezo wa mwisho wa msimu.

Mbali na ushindani wa ligi, Davids aliiongoza Simba hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup), ambapo walipoteza dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Licha ya kutotwaa mataji, alisifiwa kwa kuibadilisha Simba na kuirejesha katika kiwango cha ushindani ndani na nje ya nchi.

Baada ya kuondoka Simba, Davids alirejea Morocco kuinoa Raja Club Athletic mwanzoni mwa msimu wa 2025/26. Huko alitarajiwa kuendeleza mafanikio aliyowahi kuyapata akiwa msaidizi wa Josef Zinnbauer, ambapo waliiwezesha Raja kutwaa mataji mawili bila kupoteza mchezo.

Hata hivyo, safari yake Raja haikufika mwisho wa msimu baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo mwishoni mwa Mei, hali iliyosababisha kuondoka kwake licha ya timu hiyo kuwa bado ilikuwa kwenye mbio za ubingwa wa Botola Pro.

Inaelezwa Fadlu amewasilisha mapendekezo yake kwa uongozi wa Yanga ambapo kama makubaliano yatafikiwa basi huenda akatua nchini kuwanoa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Amtaka Moalin

Taarifa kutoka vyanzo vya karibu, imedokeza kuwa katika benchi lake la ufundi, kocha huyo amemuhitaji Abdihamid Moalin kuwemo.

Moalin alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga baada ya mabingwa hao wa soka nchini kumfuta kazi Pedro Goncalves na amefanikiwa kuisaidia Yanga kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Ikumbukwe pia Moalin alikuwa kwenye benchi la ufundi la Yanga wakati Wananchi wakiichapa Simba mabao 2-0 na kutwaa taji la ligi kuu 2024/25.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’