Mshambuliaji wa Yanga Princess raia wa Rwanda Jeannine Mukandayisenga amejiunga na klabu ya Beijing Beikong ya China kwa mkataba wa miaka miwili.
Jeannine amejiunga na klabu hiyo akitokea Yanga Princess ya Tanzania. Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akithiitisha mfungaji bora huyo wa ligi kuu ya Wanawake 2025/26 kutua kunako klabu hiyo.
Jeannine alikuwa na msimu bora ndani ya Yanga Princess baada ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Wanawake kwa msimu wa 2025/26 akifunga magoli 20.
Injinia Hersi amesema Jeannine amefuata nyayo za Aisha Masaka na Clara Luvanga ambao safari ya mafanikio yao ughaibuni ilianzia Jangwani.
ADVERTISE HERE