Makosa ya waamuzi hatua zichukuliwe sasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2026
Makosa ya waamuzi hatua zichukuliwe sasa

Baada ya Simba SC kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB kufuatia ushindi dhidi ya Azam FC katika fainali iliyochezwa visiwani Zanzibar, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu matukio yaliyojiri ndani ya mchezo huo, huku Azam FC wakionesha kutoridhishwa na baadhi ya maamuzi ya mwamuzi.

Kwa mujibu wa kile kilichoonekana na viongozi wa Azam FC, klabu hiyo ilihisi kwamba haikutendewa haki katika baadhi ya matukio muhimu ya mchezo, hali iliyozua hisia kali baada ya filimbi ya mwisho.

Chimbuko la kauli zilizotolewa na mmiliki wa klabu hiyo, Jamal Bakhresa, linatokana moja kwa moja na matukio yaliyotokea uwanjani, ambapo Azam FC wanaamini kuwa Simba walipendelewa na mwamuzi wa mchezo, huku upande wao ukionekana kukosa haki katika maamuzi kadhaa ya muhimu.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Azam FC walichukua hatua ya kugoma kuvaa medali za ushindi wa pili, jambo lililozua mjadala zaidi miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Tukio hilo limeongeza mvutano kuhusu ubora wa waamuzi wetu, huku wadau mbalimbali wakiendelea kuitaka mamlaka husika kupitia upya mfumo wa uendeshaji wa waamuzi ili kuhakikisha usawa na uwazi vinazingatiwa katika mashindano yote.

Msimu uliopita Yanga walisimama kidede kupambana na kile kilichokuwa kinaonekana matukio ya upendeleo kwa baadhi ya timu kupitia maamuzi ya ndani ya mamlaka za soka nchini pamoja na waamuzi.

Msimamo wao ulipelekea kuondolewa kwenye nafasi zao kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto, Mtendaji Mkuu Almas Kasongo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao.

Azam Fc nao wameweka msimamo kuwa msimu ujao watapambana na waamuzi 'jino kwa jino' kuhakikisha hawaonewi tena na kama wataona hakuna mabadiliko, Bakhresa amesema wanaweza kuhamia ligi ya Zanzibar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’