Baadhi ya wazee wa klabu ya Yanga SC wametoa ujumbe kwa mashabiki wa Simba SC wakiwataka warejee Jangwani kuchukua "uchafu" walioacha baada ya paredi lao juzi.
Wazee hao wa klabu kongwe zaidi nchini, wamesema Jangwani ni eneo lenye thamani kubwa kwa mashabiki na wanachama wa Yanga hivyo linapaswa kuheshimiwa.
Wazee wametoa siku tatu kwa mashabiki wa Simba kuhakikisha "uchafu" walioacha umeondolewa, wakisisitiza kuwa Jangwani ni eneo la matumizi ya wananchi na si mahali pa kuacha uchafu.
Matukio hayo ya kushangaza yalijitokeza juzi pale kundi la mashabiki wa Simba waliokuwa kwenye paredi la klabu hiyo kuvamia eneo ambalo uwanja wa Yanga unajengwa na kujisaidia haja ndogo na wengine bila ya aibu kujisaidia haja kubwa.
Hata hivyo inaelezwa hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa Simba kufanya tukio la aina hiyo. Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Hassan Dalali aliwahi kukumbwa na kadhia kama hiyo walipomvamia nyumbani kwake wakishinikiza ajiuzulu.
Baada ya mavutano na hapa na pale, Dalali amewahi kunukuliwa na vyombo vya habari akitoa ushuhuda wake kundi hilo liktawanyika maeneo mbalimbali ya nyumba yake na kujisaidia haja kubwa!