Wachezaji Mohamed Doumbia, Moussa Balla Konte, Offen Chikola, Ecua Celestin na Denis Nkane wamemaliza mikataba yao ya mikopo.
Doumbia alikuwa na wakati mzuri akiitumia Marumo Gallants ya Afrika Kusini wakati Ecua akiitumikia JS Kabylie ya Algeria.
Awali kulikuwa na makubaliano kwa Kabylie kumsajili Ecua moja kwa moja lakini klabu hiyo imeachana na mpango huo baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.


Inaelezwa uongozi wa Yanga ulishafungua mazungumzo nae kwa ajili ya kusitisha mkataba wake sambamba na Doumbia ambaye anaweza kujiunga moja kwa moja na Marumo.
Nyota wengine Conte, Nkane na Chikola bado wana mikataba na Yanga hatma zao kuelekea msimu ujao zitafahamika.

Rais wa Yanga Injia Hersi Said ameahidi maboresho makubwa ya kikosi ili kuhakikisha msimu ujao Yanga inakuwa imara zaidi ili kurejesha mataji yote waliyopoteza msimu huu na kufanya vyema zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa(CAFCL).