Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Jeannine Mukandayisenga, ametambulishwa rasmi na klabu ya Wuhan Jiangda Women's Football Club ya nchini China, akianza rasmi ukurasa mpya wa maisha yake ya soka baada ya kung'ara katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Jeannine anaondoka Yanga Princess baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili yenye mafanikio makubwa, ambapo alijidhihirisha kama mmoja wa washambuliaji hatari zaidi katika soka la wanawake nchini Tanzania.
Katika msimu wa 2025/26, nyota huyo wa Rwanda alimaliza akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, akitoa mchango mkubwa kwa Yanga Princess kupitia mabao na kiwango chake bora uwanjani.
Mafanikio hayo yalimfungulia mlango wa kuhamia katika moja ya ligi zenye ushindani mkubwa duniani.
Anaungana na nyota wengine waliowahi kupata mafanikio wakitoka Yanga Princess kama Aisha Masaka na Clara Luvanga