Matthew Silva awaaga mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2026
Matthew Silva awaaga mashabiki Yanga

Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Young Africans SC, Matthew Silva, ameaga rasmi mashabiki wa timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika, huku akieleza kuwa anaondoka akiwa na kumbukumbu nzuri na uzoefu mkubwa alioupata akiwa ndani ya klabu hiyo yenye historia kubwa nchini Tanzania.

Silva alitoa ujumbe wa kuaga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, akieleza fahari yake ya kumaliza safari yake Yanga akiwa katika hali aliyokuwa akiitamani kama mtu mwenye moyo wa kujituma, mwenye nidhamu, anayependa kazi na mtaalamu wa soka.

"Ninaondoka katika klabu hii kubwa ya Afrika nikiwa na kumbukumbu nzuri tu na uzoefu uliyonijenga zaidi, kunifanya nikue na kuniandaa kwa hatua zinazofuata," aliandika Silva.

Kocha huyo alisema lengo lake lilikuwa kuondoka Yanga akiwa ameacha taswira nzuri kama mtu mwenye moyo wa kusaidia, mwenye heshima, bidii na kujitolea, akiamini kuwa hilo limetimia.

Silva pia aliwashukuru viongozi wa Yanga, benchi la ufundi, wachezaji na hasa aliyekuwa kocha wa Yanga Pedro Soares Gonçalves kwa kumpa nafasi ya kufanya kazi katika klabu hiyo.

"Kwa kocha Pedro, asante sana kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi na wewe katika klabu hii kubwa. Ni kipindi gani kizuri kuwa hapa na ni kazi kubwa tuliyoifanya pamoja, hasa baada ya kuwa mchezaji wako miaka 20 iliyopita," alisema.

Katika ujumbe wake, Silva aliipongeza bodi ya uongozi wa Yanga kwa juhudi zake za kuendeleza klabu na kuweka mazingira ya kupigania mafanikio makubwa.

Aliwapongeza pia wachezaji kwa kujituma uwanjani na kufanikisha malengo ya timu, akisema walikuwa na ubora na dhamira ya kufanya mambo makubwa.

Matthew anaondoka akiacha kumbukumbu nzuri kwa Wananchi, amehusika kwenye mataji mawili kombe la Mapinduzi na ligi kuu ya NBC.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’