Kindoki kipa wa zamani Yanga afariki Dunia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2026
Kindoki kipa wa zamani Yanga afariki Dunia

Tasnia ya soka nchini hasa mashabiki wa Yanga wamekumbwa na simanz kubwa leo baada ya kifo cha aliyekuwa mlinda lango wa zamani wa Yanga SC, Clause Kindoki, ambaye amefariki dunia kutokana na ajali ya barabarani huko Kinshasa DR Congo.

Kindoki amefariki jana, Jumamosi, Julai 11, 2026, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la FA.

Kwa mujibu wa meneja wa zamani wa mshambuliaji Fiston Mayele, Nestor Mutuale, Kindoki alikuwa akiitumikia klabu ya Bustras kama kocha wa makipa. Timu hiyo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Et Dauphin ya Goma katika mchezo uliochezwa jijini Kinshasa.

Mutuale amesema kuwa baada ya mchezo huo, Kindoki hakurejea na basi la timu kama ilivyokuwa kwa wachezaji na benchi la ufundi. Badala yake, aliamua kutumia usafiri wa bodaboda, ambapo baadaye alipata ajali mbaya iliyohusisha lori la mizigo.

Clause Kindoki anakumbukwa kwa kuitumikia Yanga SC akiwa mmoja wa makipa wa klabu hiyo kabla ya kurejea DR Congo, ambako aliendelea kutoa mchango wake katika maendeleo ya soka kupitia nafasi ya ukocha wa makipa.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa familia yake, marafiki, pamoja na wadau wa soka nchini DR Congo na Tanzania. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Kindoki alijiunga na Yanga mnamo mwaka 2018, akisajiliwa kutoka klabu ya AC Leopards ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) chini ya aliyekuwa kocha wa Yanga wakati huo, Mwinyi Zahera.

Aitua nchini sambamba na mshambuliaji Heritier Makambo, ambapo alicheza nchini kwa msimuu mmoja kabla ya kurejea kwao Dr Congo.

Mwenye ez Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Peponi AMEN..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’