Kanuni ya mgeni kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi yarekebishwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2026
Kanuni ya mgeni kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi yarekebishwa

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametangaza kufutwa kwa kanuni iliyokuwa ikiziruhusu timu wageni kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi kabla ya siku ya mchezo.

Amesema kuanzia sasa utaratibu huo utatumika tu pale timu itakapokuwa inacheza kwenye uwanja husika kwa mara ya kwanza.

Karia amesema mabadiliko hayo yanalenga kuboresha uendeshaji wa mashindano na kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kutokana na utekelezaji wa kanuni hiyo. Kwa mujibu wake, hakuna sababu ya timu kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja ambao tayari ina ufahamu nao kutokana na kucheza mara kwa mara.

Kanuni hiyo imekuwa chanzo cha migogoro katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, hususani dabi za Simba na Yanga, ambapo kumekuwa na mvutano kuhusu haki ya timu mgeni kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi.

Wengi wanakumbuka kile kilichotokea March 08 2025 mechi namba 184 pale Simba walipoweka mpira kwapani wakidai kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho uwanja wa Benjamin Mkapa.

Lakini pia kuna matukio yanayohusiana na masuala la kishirikina ambapo baadhi ya timu hutumia muda huo kuyafanya. Hatua hii ya TFF itakuwa pigo kubwa kwa wale waliowekeza kwenye matumio ya aina hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
21m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’