Mlinda lango Hussein Masalanga amemaliza mkataba wa mkopo na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga sasa akihusishwa kutua klabu ya Geita Gold Fc.
Masalanga alijiunga na Yanga mwezi Januari 2026 kwa mkopo wa miezi 6 akitokea klabu ya Singida BS.
Aklitua kuchukua nafasi ya Aboubakar Khomein ambaye alipata majeraha yaliyomuweka nje ya dimba kwa zaidi ya wiki 10.
Khomein tayari amepona majeraha na pengine huenda akarejea kikosini katika maandalizi kuelekea msimu mpya 'pre-season'.
Masalanga anaondoka Yanga akiwa na medali ya ubingwa wa ligi kuu ya NBC akiwa sehemu ya kikosi kilichofanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo.
ADVERTISE HERE