Manqoba ahitaji mawinga wawili Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2026
Manqoba ahitaji mawinga wawili Afrika Kusini

Klabu ya Yanga imeanza enzi mpya chini ya kocha raia wa Afrika Kusini, Manqoba Mngqithi ambaye anaendelea kuweka sawa mipango yake kabla ya kutua nchini kuanza majukumu yake.

Kocha huyo wa zamani wa Golden Arrows ana jukumu la kuendeleza mafanikio ya Yanga ndani ya nchi pamoja na kuifanya timu hiyo kuwa tishio zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ahitaji mawinga wawili

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa iDiski Times wa Afrika Kusini, Yanga iko kwenye mchakato wa kuwasajili wachezaji wawili mawinga wanaocheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) ili kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Mchezaji wa kwanza ni Thulani Gumede, ambaye anaitumikia Richards Bay. Gumede amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa klabu hiyo kutokana na uwezo wake wa kucheza pembeni na kuchangia katika safu ya ushambuliaji.

Mchezaji wa pili ni Justice Figareido wa Chippa United. Winga huyo mwenye uzoefu wa kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Eswatini amecheza zaidi ya mechi 20, huku akiwa amefunga mabao 11 na kutoa pasi nane za mabao katika mechi 111 za Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Ripoti zinaeleza kuwa wachezaji wote wawili wanaonyesha nia ya kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania wakisubiri kukamilika kwa michakato ya usajili baina ya Yanga na klabu zinazowamiliki.

Iwapo usajili huo utakamilika, Yanga itaongeza nguvu kubwa katika maeneo ya pembeni, jambo litakalompa Manqoba Mngqithi chaguo zaidi wakati akijiandaa kwa mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
19m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’