Baada ya mkataba wake kumalizika, inaelezwa uongozi wa klabu ya Yanga uko kwenye mazungumzo na kiungo mkongwe Salum Abubakar 'Sure Boy' ili kumpa mkataba mpya.
Kumekuwa na mapendekezo kutoka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa mabingwa hao wa nchi wakitaka Sure Boy asaini mkataba mpya licha ya nafasi yake finyu kwenye kikosi cha kwanza.
Msimu uliopita Sure Boy hakuonekana mara kwa mara uwanjani lakini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, alifanya kikamilifu jukumu la ki-uongozi, kuwahamasisha na kuwaunganisha wenzake katika nyakati ngumu.
Kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya JKT Tanzania, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alifichua kuwa Sure Boy alifanya kazi kubwa kuhakikisha wachezaji wanarejea kumaliza mchezo huo kwa nguvu baada ya mapumziko kufuatia jeraha baya alilopata kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua.
Ni wazi Sureboy ana nafasi kubwa ya kuongezewa mkataba na kuendelea kusalia kwa mabingwa hao wa nchi licha ya kupokea ofa kutoka kwa timu mbalimbali zinahitaji huduma yake